Sisi kama wanachama, wachangiaji, na viongozi tunaahidi kuwa ushirikiaji katika jamii yetu uwe wenye usio na unyanyasaji kwa yeyote, bila kujali umri, umbo la mwili, ulemavu unaoonekana, au usioonekana, kabila, sifa za jinsia, utambulisho wakijinsia na kujieleza, kwa kiwango cha ustadi, elimu, hali ya jamii-kiuchumi, uraia, muonekano binafsi, rangi, tabaka, rangi, dini, au utambulisho wa kijinsia na mwelekeo wa kimapenzi.
Tunaahidi kuchukua hatua na kuingiliana kwa njia zinazochangia uwazi, unao karibisha, utofauti, ujumuishi na yenye afya.
Mifano ya tabia ambayo inachangia mazingira mazuri kwa ajili ya jamii hii ni yafuatayo:
Mifano ya tabia isiyokubalika ni yafuatayo:
Viongozi wa jumuiya wana wajibu wa kufafanua na kutekeleza viwango vyetu vya tabia yanayokubalika na kuchukua hatua zinazofaa kwa haki za kurekebisha na kujibu tabia yoyote ambayo wanaona haufai, vitisho, yanayokera, au madhara.
Viongozi wa jumuiya wana haki na wajibu wa kuondoa, kuhariri au kukataa maoni, ahadi, msimbo, uhariri wa “wiki”, masuala, michango mingine ambayo haiambatani na kanuni hii ya maadili na kutawasilisha sababu za kukadiria maamuzi inapofaa.
Kanuni hii ya Maadili inatumika ndani ya nafasi zote za jumuiya, na pia inatumika pale mtu binafsi anapowakilishwa rasmi kijumuiya katika maeneo ya umma. Mifano ya kuwakilisha jumuiya yetu ni pamoja na kutumia anwani rasmi ya barua pepe, kuchapisha kupitia akaunti rasmi ya mitandao ya kijamii, au kupitia wakilishi mteule katika tukio cha mtandao au nje ya mtandao.
Matukio ya matusi, unyanyasaji, au tabia nyingine isiyokubalika inaweza kuripotiwa kwa viongozi wa jamii wanaohusika na utekelezaji katika conduct@ethicalsource.dev. Malalamiko yote yatafwatiliwa na kuchunguzwa mara moja na kwa haki.
Viongozi wote wa jumuiya wana wajibu wa kuheshimu faragha na usalama wa mwandishi wa ripoti ya tukio.
Viongozi wa jumuiya watafuata mwongozo huu ya athari kwa Jumuiya katika kubainisha matokeo ya kitendo chochote wanachokiona kinakiuka Kanuni hii ya Maadili:
Athari kwa jamii: Matumizi ya lugha isiyofaa au tabia nyingine inayozingatiwa kuwa usio wa utaaluma au usiokubalika katika jamii.
Matokeo: Onyo la faragha, lililoandikwa kutoka kwa viongozi wa jumuiya, kutoa uwazi kuhusu asili ya ukiukaji na maelezo ya kwa nini tabia haikuwa sawa. Msamaha wa umma unaweza kuombwa.
Athari kwa jamii: Ukiukaji kupitia tukio au mfululizo mmoja ya vitendo usiofaa.
Matokeo: Onyo lenye matokeo ya tabia ilioendelezwa. Hakuna kuungana na waliohusika, ikiwemo mwingiliano usio ombwa na wale wanaotekeleza Kanuni za Maadili, kwa muda maalum. Hii inajumuisha kuepuka mwingiliano katika nafasi za jumuiya vile vile katika za nje kama mitandao ya kijamii. Kukiuka masharti haya kunaweza kukusababishia marufuku ya muda au wakudumu.
Athari kwa jamii: Ukiukaji mkubwa wa viwango vya jumuiya, ikijumuisha kudumu kwa tabia zisizofaa.
Matokeo: Marufuku ya muda kwa aina yoyote ya mwingiliano au mawasiliano ya hadharani na jamii kwa muda maalum. Hakuna mwingiliano wa kibinafsi au wa uma na watu wanaohusika, ikiwemo mwingiliano usio ombwa na wale wanaotekeleza Kanuni za Maadili, inaruhusiwa katika kipindi hiki. Kukiuka masharti haya kunaweza kusababisha marufuku ya kudumu.
Athari za Jumuiya: Kuonyesha mtindo wa ukiukaji wa viwango za jumuiya, ikiwa ni pamoja na tabia isiyofaa uliyodumu, unyanyasaji wa mtu binafsi, mwenendo wa uchokozi au kudharau matabaka ya watu binafsi.
Matokeo: Marufuku ya kudumu kutoka kwa aina yoyote ya mwingiliano wa umma ndani ya jamii.
Kanuni hii ya Maadili yatokana na Agano la Wachangiaji, toleo la 2.1, yapatikana katika https://www.contributor-covenant.org/version/2/1/code_of_conduct.html.
Miongozo ya Athari kwa Jamii ilichochewa na Ngazi ya Kutekeleza Kanuni ya Uendeshaji wa Mozilla..
Kwa majibu ya maswali ya kawaida kuhusu kanuni hii ya maadili, angazia kwa ‘Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara’ https://www.contributor-covenant.org/faq. Matafsiri yapatikana katika https://www.contributor-covenant.org/translations.